APRILI: KWA UTAMADUNI WA AMANI NA USIO NA VURUGU

APRILI: KWA UTAMADUNI WA AMANI NA USIO NA VURUGU

????

Kuishi, kuzungumza na kutenda bila jeuri haimaanishi kukata tamaa, kupoteza au kuacha chochote. Inamaanisha kutamani kila kitu. Kama Mtakatifu John XXIII alivyosema miaka 60 iliyopita katika waraka kumbakumba Pacem in Terris, (Amani Ulimwenguni) vita haina mantiki, ni zaidi ya kutofikiri. Vita yoyote, mapigano yoyote ya silaha, daima huisha kwa wote kushindwa. Tujenge utamaduni wa amani. Tukumbuke hata katika kujilinda, amani ndio lengo kuu. Na kwamba amani ya kudumu inaweza tu kuwa amani isiyo na silaha. Hebu tusifanye vurugu katika maisha ya kila siku na katika mahusiano ya kimataifa, huu uwe mwongozo wa matendo yetu. Na tuombe kwa ajili ya kuenea zaidi kwa utamaduni wa kutotumia mabavu, ambao unahusisha utumiaji mdogo wa silaha, kwa serikali na raia.

Advertisement

LEAVE YOUR COMMENT

More Catholic Videos