MACHI: KWA WAATHIRIWA WA UNYANYASAJI

MACHI: KWA WAATHIRIWA WA UNYANYASAJI

????

Katika kukabiliana na kesi za unyanyasaji, hasa kwa wale waliotendewa na washiriki wa Kanisa, haitoshi kuomba msamaha. Kuomba msamaha ni muhimu, lakini haitoshi. Kuomba msamaha ni vyema kwa ajili ya waathirika, lakini wao ndio wanapaswa kuwa "katikati" ya kila kitu. Maumivu yao na majeraha yao ya kisaikolojia yanaweza kuanza kupona ikiwa watapata majibu�ikiwa zipo hatua madhubuti za kurekebisha maovu waliyoyapata na kuyazuia yasitokee tena. Kanisa haliwezi kujaribu kuficha janga la unyanyasaji wa aina yoyote. Hata kama unyanyasaji unafanyika katika familia, kwenye vilabu, au kwenye aina nyiginezo za taasisi. Kanisa lazima liwe kielelezo cha kusaidia kutatua suala hilo na kuliweka wazi katika jamii na ndani ya familia. Kanisa lazima litoe nafasi salama kwa waathirika kusikilizwa, kusaidiwa kisaikolojia, na kulindwa. Tuwaombee wale ambao wameteseka kwa sababu ya maovu waliyotendewa kutoka kwa washirika wa Kanisa; wapate ndani yao Kanisa lenye jibu thabiti kwa mateso na maumivu yao.

Advertisement

LEAVE YOUR COMMENT

More Catholic Videos