FEBRUARI: KWA PAROKIA

FEBRUARI: KWA PAROKIA

????

Wakati mwingine Mimi hufikiri kwamba tunapaswa kuweka alama kwenye mlango wa parokia inayosema, 'Kiingilio bure.' Parokia zinapaswa kuwa jumuiya zinazounganishwa kwa karibu, bila urasimu, zinazojikita kwa watu- mahali ambapo zawadi ya masakramenti yanapatikana. Ni lazima ziwe tena shule za huduma na ukarimu, na milango yao wazi kila mara kwa wale ambao wametengwa. Na kwa wale wamejumuishwa. Kwa wote. Parokia sio kilabu ya wachache, ambayo hutoa aina fulani ya mali ya kijamii. Tafadhali, tuwe na ujasiri. Hebu sote tufikirie upya mtindo wa jumuiya zetu parokiani. Tuombe kwamba parokia, ziweke komunyo -ushirikiano wa watu, ushirika wa kikanisa �kipaumbele, ziweze kuzidi kuwa jumuiya za imani, za undugu na za kukaribisha wenye uhitaji mkubwa.

Advertisement

LEAVE YOUR COMMENT

More Catholic Videos